Makamu wa Rais mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango azindua mradi wa kufua umeme Makete, IJangala mini hydropower wenye kilo watt 360.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri, wabunge, Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Viongozi wa Dini, Viongozi mbalimbali wa vyama na taasisi mbali mbali.
Mradi huo ulio chini ya kanisa la KKKT umegharimu zaidi ya bilioni tatu mpaka sasa.
Katika kuhakikisha Mradi huu unafanikiwa na kuleta matokeo,zaidi ya makampuni matano yameshiriki na mshauri elekezi wa mradi huo ni kamuni ya Mcb consultancy Bureau iliyopo chini ya Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia (MUST)
Makamu wa rais mhe. Dkt. Isidor Philipo Mpango aliwashukuru wote waliofanikisha kuzindua mradi huo hasa Kanisa la KKKT kwa kupata maono hayo.
Pia amewashukuru wakandarasi pamoja na mshauri Elekezi wa mradi, mhe. Makamu wa rais ameeleza nia ya serikali ni kuleta maendeleo kwa wananchi na kuwataka wananchi kutumia vyema fursa za miradi inayoanzishwa. Aidha amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano na madhehebu yote ya dini ili kuendelea kuleta maendeleo ya kwa taifa.
Katika Uzinduzi huo Prof. Zacharia Katambara kutoka chuo kikuu cha Must akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mhe. Makamu wa rais amesema mradi huo unategémewa kua msaada kwa taifa kwasababu utapunguza changamoto ya umeme katika taifa kwani unaelekzwa katika grid ya Taifa.
Nae mkurugenzi wa kampuni ya Mcb Mhandisi Ivor Ndimbo amesema wao kama washauri elekezi watahakikisha wanasimamia kikamilifu mradi huo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.