Hali ilivyo katika Ofisi Ndogo ya Chama cha Mapinduzi ya Makao Makuu na mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho.
Itakumbukwa mabadiliko ya wajumbe hao yamefanyika hivi karibuni kupitia Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika kikao chake maalum kilichoongozwa na Mwenyekiti wake na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Wajumbe waliofika ni Amos Makalla, Jokate Mwegelo, Ally Hapi na John Mongela.