Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariam Mwinyi ameshiriki matembezi na mbio za Marathon katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani.
Katika kilele cha matembezi hayo Mama Mariam Mwinyi alisema Serikali ya Zanzibar imechukuwa hatua mbalimbali kwa lengo la kukomesha vitendo vya udhalilishaji kama vile kutunga sheria zenye adhabu kali bila dhamana ili kuondoa vitendo hivyo.
Ameipongeza Mahakama kwa jitihada inazochukua kushughulikia kesi za udhalilishaji, miongoni mwa juhudi hizo ni kuundwa kwa Mahakama maalumu ya kushughulikia makosa ya udhalilishaji. Mwaka 2022 Mahakama ilikuwa na jumla ya kesi za udhalilishaji 1,260 na katika hizo kesi 867 ambazo ni sawa na asilimia 68.9% ziliamuliwa.
Katika maadhimisho hayo Mama Mariam aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib, Jaji Mkuu Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Jaji Mkuu Tanzania Mhe. Ibrahim Khamis Juma.