Mbunge Ester Bulaya amezindua rasmi mashindano ya ‘Bulaya Cup 2023’ kwa timu za wasichana na wavulana kwa wilaya Bunda ambapo mashindano yatajumuisha zaidi ya timu 20.
Katika ufunguzi huo timu ya wasichana ya Bunda queen imeshinda kwa goli tatu kwa sifuri dhidi ya timu ya wasichana ya Bunda girls, mchezo uliohudhuliwa na mdhamini wa mashindano Ester Bulaya pamoja na viongozi wa soka mjini Bunda.
Baada ya mchezo wa ufunguzi kikamilika Ester Bulaya akajibu maswali ya Waandishi wa habari waliotaka kufahamu maoni yake baada ya kuanza kwa mashidano hayo
“Mmeshuhudia vipaji kutoka Bunda, ndoto yangu nikuona tunaendelea kutoa wachezaji wengi kwenda ligi kubwa kutoka mkoa wa Mara, mpira wa miguu kwa wasichana ni kama unasahaulika nimeona tupate burudani pande zote”
Mashindano ya ‘Bulaya Cup 2023’ yatadumu kwa muda wa mwezi mmoja huku gharama za mashindao hayo ni zaidi ya milioni 20, kutoka mfukoni kwa Mbunge Ester Bulaya.