Miili ya Ndugu watatu wa Familia moja ambao walifariki usiku wa kuamkia August 03,2023 baada ya gari (Toyota Prado) walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam, imeagwa leo Lugalo Golf Course, Dar es salaam kabla ya kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kondo Tegeta.
Miili ya Watoto hao wa Mr. Hashim Msuya na Mkewe inayoagwa leo ni wa Siah Hashimu Msuya (53), Diana Sukulu Mageta (47) na Dkt. Norah Msuya Mumburi (45), mwili wa Kaka yao (Dereva wa Prado) ambaye walipata nae ajali hiyo, Neech Hashim Msuya ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Benki ya ABSA tayari umeshazikwa Jumapili katika Kijiji cha Msangeni Ugweno Wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila pamoja na Viongozi wengine wameungana na waombolezaji wengine kuaga miili hiyo.