Katika kumbukizi ya kifo cha Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mbezi Beach wamefanya misa ya kumuombea Hayati Karume.
Hayati Karume alizaliwa mwaka 1905 na kufariki April 7, 1972 kwa kupigwa risasi.
Salum Viduka ambaye ni Mratibu wa Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia Suluhu Hassan amesema kwa kushirikiana na kanisa hilo wamefanya Misa ya kumuombea Karume kutokana na kuongoza mapambano ya kupigania haki ya Watanzania.
“Sheikh Karume akuangalia dini, rangi wala kabila bali aliangalia Watanzania kwanza na kutanguliza maslahi yetu ndio maana leo hii anaombewa dua kwa kila dini ikiwemo hapa Kanisani, yupo mioyoni mwetu na tutaendelea kumkumbuka daima,”.
Naye Lilian Rwebangila ambaye ni muumini wa kanisa hilo amesema “Kwetu Mzee Karume ni shujaa na tutaendelea kumuombea kwa sababu aliongoza mapinduzi kupigania amani na haki zetu kama Watanzania,”.