Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Iringa Injinia Fatma Rembo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, amekabidhi pikipiki nne kwenye wilaya za mkoa wa Iringa ili kusukuma maendeleo.
Pamoja na pikipiki hizo, amekabidhi Shilingi 1,000,000 kwa wilaya hizo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo.
Wilaya zilizopewa pikipiki hizo ni Mufindi, Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijijini.
Akikabidhi pikipiki hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred Daud Yasin Mlowe amempongeza Injinia Fatma huku akisisitiza suala kila kiongozi kutekeleza wajibu wake.
Comred Yassin amewaomba wazitunze pikipiki hizo ili ziendelee kusaidia kazi mbalimbali na uchumi.
“Tuendelee kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii. Tuendelee kumsemea,” amesema Comred Yassin.
Injinia Rembo amesema baada ya ziara yake kwenye wilaya zote Mkoani Iringa aliahidi kukabidhi pikipiki na fedha kwa ajili ya matofari.
“Pia tuendelee kumuunga mkono Rais Samia kwa kuchapa kazi na kumsemea mazuri , pikipiki hizi zitatusaidia sana kwenye changamoto za kiuchumie,” amesema Rembo.
Awali, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Comred Salim Asas Abri alisisitiza upendo.
“Kina mama mpendane, mkiyumba nyie chama kimeyumba pia, mkiona mwenzio amefanya jema mpongeze. Pia muwe mstari wa mbele kumtetea mwanamama mwenzenu”- Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Comred Zainab Mwamwindi alizungumzia umoja na mshikamano miongoni mwao.
“Nampongeza Fatma na kwa kweli tuendelee kushikamana, tufanye kazi kwa umoja na upendo,” amesema Mwamwindi.