Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa Mashiriki kwenye zoezi la kupanda miti 300 katika Shule ya Sekondari Kihere ikiwa ni jitihada za serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchini .
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mgandilwa anasema kuwa sababu kubwa inayopelekea mabadiliko ya tabia ya nchini ni kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanya na jamii hivyo zoezi hilo ni kuwajengea uwevijana kufahamu umuhimu wa utuanzaji wa mazingira.
“Unajua kwasasa dunia na Tanzania tunakabiliwa sana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi sasa tunaendeleoa na kampeni ya uhamasishaji hususani ni kwavijana hivyo tumeona kimsingi wao tuwajengee uelewa wa umuhimu wa utunzaji wa mzingira na upandaji wa miti kwani kwa kisi kikubwa miti imeadhirika sana hivyo tunawajengea uelewa wanafunzi kuwa na ile kaulimbiu ya kusoma na mti wangu”- Hashimu mgandilwa.
Aidha alisema kuewa kupitia hiki kipindi ambacho tunakwenda nacho kwa kipindi cha miaka mitatu mnne ambayo tunaenda nayo ni kuhakikisha kila eneo ambalo ni eneo la wazi linalo stahili kuwa na miti kuhakikisha miti inapandwa ili kuwa na Tanga ya kijani.
Kwa upande wake Mwajabu Mkungu ambaye ni Afisa Maliasili na Uhifadhi wa mazingir ndani ya jiji la Tanga alisema kuwa katika zoezi hilo wamefanikiwa kupanda miti Zaidi ya mia mbili ambazo zoezi hilo linafanyika ikiwa ni moja ya mikakati iliyopo ya upandaji miti kama SHERIA inavyotaka kujikita kwenye upandaji wa Miti ambapo hadi sasa kama jiji la Tanga wamesha panda miti kwenye maeneo mbalimbali kama Hospitali,Mashuleni pamoja na Ofisi Mbalimbali za Serikali.