Ni July 24, 2023 ambapo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao ameshiriki ufunguzi wa Baraza la Kawaida la UVCCM Mkoa wa Pwani.
Aidha Bw. Ramadhan Mlao amesitiza kuwa chaguzi zimekwisha sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa nguvu na umoja mkubwa pia amewashukuru wajumbe Kwa kumuamini na Kumchagua kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu UVCCM Taifa, Hata hivyo amewaambia hata yeye alikuwa Miongoni mwa Wa Wajumbe wa Baraza lililopita.
Lakini pia amewataka Wenyeviti wa UVCCM Wilaya Zote Katika Mkoa wa Pwani Kufanya Ziara za Utendaji Kazi Katika Maeneo Yao.
Hata Hivyo Ndugu MNEC Amekanusha na Kuwataka Vijana wakanushe Maneno ya Uzushi yanayo Semwa Mtaani Kuwa Bandari Imeuzwa na Nchi Imeuzwa, Amesema Hakuna Kitu Cha Namna Hiyo na M.kiti wa CCM Taifa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi Kufanya kitu kama Hicho katika Taifa lake.
Amewaomba Watanzania Wote Kupuuza Usemi Huo unao Vumishwa Mtaani. MNEC Amesisitiza Vijana Kuepuka na Kuhubili Udini, Ukabila Wala Ukanda Baina yetu Kwani Kwa Kufanya Hivyo Tutasababisha Migogoro.
Pia Ndugu MNEC Amemshukuru Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Kuendelea Kuwaamini Vijana Katika Serikali yake na Kuwateua Vijana zaidi ya 75% Ili wakamsaidie Kazi Mbalimbali. Ndugu MNEC Amesema Kwa Vijana Wote walioaminiwa Wakafanye Kazi Kwa weledi, Nidhamu na Kwa Maarifa Yao yote Ili kuendelea Kulinda Imani Zao za Kuaminiwa Kwani Kwa Kufanya Hivyo Itawasaidia Vijana.