Picha ya rapper wa Canada, Rapper Tory Lanez imeachiliwa ikimuonesha akiwa amesimamishwa katika gereza la serikali kufuatia kukutwa na hatia ya kumpiga risasi msanii mwenzake wa hip-hop Megan Thee Stallion.
Lanez, 31, alipatikana na hatia ya kumpiga risasi Megan na alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na hakimu.
Matumaini yake ya kutoka gerezani yalififia hivi majuzi baada ya hakimu kukataa rufaa yake, akitaja sababu za ukiukaji wa amri yake ya mahakama, hatia ya uhalifu wa kikatili, na uraia usio wa Marekani kuwa sababu.
Tory Lanez hivi majuzi alihamishiwa kwenye gereza la serikali na ilibidi apige picha mpya kabla ya kuingia jela.
Inasemekana aliingia mnamo Jumanne Septemba 19, katika Gereza la Jimbo la Kern Kaskazini huko Delano, California, lililoko takriban maili 145 kutoka Los Angeles.
Lanez alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kumpiga risasi rapa Megan Thee Stallion mguuni.
Kabla ya kuhukumiwa kwake, waendesha mashtaka walikuwa wamemtaka hakimu huyo ampe rapper huyo miaka 13 jela.
Mahakamani, alishtakiwa kwa kumtia kiwewe Megan tena na machapisho kadhaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kesi hiyo na kuchochea hasira kutoka kwa watu mtandaoni kwake kwa kufanya hivyo.