Ni Agosti 18, 2023 ambapo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohamed Ali Kawaida (MCC) akiongozana na kamati ya Utekelezaji katika ziara yake Mkoa wa Mjini Unguja ametembelea na kuzindua Kisima Cha Maji safi na Salama kupitia fedha za mfuko wa Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae, kilichopo Migombani.
Ndugu Kawaida yupo Mkoa wa Mjini Unguja kuendelea na ziara yake ya kikazi ambapo ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM-Taifa, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi wanaowakilisha kundi la Vijana na Wabunge wa Vijana.
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana, kutembeleabna kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali Visiwani Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025 pamoja na miradi ya Chama na Jumuiya zake pamoja na kutatua Changamoto mbalimbali zinazowakabili Vijana.