Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akiwa sambamba na mke wake Salma Kikwete, akielekea kupanda treni ya Umeme ya SGR, kuelekea jijini Dodoma kushiriki Mkutano maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, unaotrajiwa kufanyika Januari 18 na 19, 2025.
Aidha katika treni hiyo wamepanda pia wasanii mbalimbali wakiwemo wa filamu, vichekesho na watu wenye ushawishi katika mitandao ya jamii (Influencer).
Dkt. Kikwete na wasanii hao mbalimbali wa filamu wanaungana na kundi la wajumbe 750 wa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa ambao wapo pia wamesafiri na treni hiyo kuelekea Dodoma kwaajili ya mkutano huo.