Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping kando ya Mkutano wa BRICS unaofanyika Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini leo tarehe 24 Agosti, 2023.
Moja ya mambo yaliyojiri kwenye mkutano huo leo ni Viongozi wa kundi la Mataifa yanayoinukia kiuchumi la BRICS kukubaliana kuongeza idadi ya Wanachama na kuidhinisha masharti kwa Nchi nyingine kujiunga na kundi hilo ambapo Nchi sita za Argentina, Misri, Iran, Ethiopia, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimekaribishwa kuwa Wanachama wapya wa BRICS.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye ni Mwenyeji wa Mkutano huo wa Kilele wa BRICS amesema Nchi hizo zitajiunga ifikapo rasmi January mwakani.
BRICS inaundwa na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini ambapo mkutano wake unaendelea Johannesburg na Viongozi wa Mataifa mbalimbali wamekaribishwa kushiriki.