Ni Machi 14, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Tamasha la Wanawake Sekta ya Fedha ambalo limefanyika Kizimkazi, Zanzibar.
Tamasha hilo limeandaliwa na Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha (TAWiFA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwanamke Initiatives (MIF) pamoja na TIRA.