Ni April 24, 2024 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan leo amewatunuku nishani viongozi mbalimbali katika shamrashamra za miaka 60 ya Muungano wa Tanzania Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.Mmoja wa Waandishi wa Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahamoud Thabit Kombo akizungumza kabla ya uzinduzi wa Kitabu hicho kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa vitabu vya Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwa Mama Hasna Kawawa mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Rashid Mfaume Kawawa (kulia) na Mama Fatuma Jumbe Mjane wa Rais wa Pili wa Zanzibar Hayati Aboud Jumbe Mwinyi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 60 ya Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Kitabu cha Safari za Picha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.