Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi kwa manufaa ya mkoa na Nchi kwa ujumla.
RC Kindamba ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea baadhi ya viwanda ndani ya jiji la Tanga amepambo alisema nia ya Serikali ni kuona wawekezaji wanafanya shughuli zao pasipo kuwa na vikwazo lakini pia wananchi wananufaika na uwepo Viwanda hivyo kwa kupata ajira.
“Nia ya Serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kufanya shughuli zao bila ya usumbufu huku wakiendelea kulipa kodi kwa hiari na watu wetu kupata fursa za kuajiriwa” amesema Kindamba
Aidha Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwa wawekezaji kwa mwaka 2022 wawekezaji waliweza kuchangia kwa kulipa kodi na tozo kwa serikali takribani shilingi Bilioni 12.
“Nimepitia ripoti zao mwaka jana tu ukichukua tozo mbalimbali na kodi za Serikali wamechangia uchumi wa nchi yetu karibu Bilioni 12 huku wakitoa ajira za wastani takribani watu 1200” aliongeza Kindamba.
Pia mhe Kindamba amewatoa hofu wawekezaji hasa wa viwanda kuhusu suala la umeme na kuahidi kuwa mpaka kufikia Julai Mosi tatizo la umeme mkoani Tanga itakuwa Historia.
Nae Msaidizi mkuu idara ya fedha idara y kiwanda cha kuzalisha saruji cha Maweni limestone CPA Peter Shuma amesema kuwa maboresho ya bandari ya Tanga yamesaidia kurahisisha shughuli za usafiri wa saruji kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.