Taasisi ya mtetezi wa Mama ambayo ni muonganiko wa mikoa mbalimbali yenye lengo la kumsemea na kueneza miradi na maendeleo yanayofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo imeamua kufanya maandamano ya amani kwaajili ya muendelezo wa uzinduzi ambao unafanyika katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu taifa wa taasisi ya mtetezi wa Mama Neema Karume amesema dhumuni la maandamano hayo ni kwaajili ya kumpambania Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha 2025 anarudi tena kwa kishindo.