Club ya Tottenham Hotspurs leo imeonesha ilivyobadili sehemu ya uwanja wake na kuwa sehemu ya kutolea huduma kwa watu kupima maambukizi ya virusi vya corona.
Tottenham wametengeneza sehemu ya kutolea huduma hiyo underground ambako kunatumika kama maegesho ya magari.
Sehemu hiyo hiyo chini ya taasisi ya hutoaji wa huduma ya afya England (NHS), watakuwa na uwezo wa kupima watu 70 kwa siku na kutakuwa na manesi 10, muda wa kutoa huduma hiyo itakuwa saa nne asubuhi hadi saa nane mchana Jumatatu hadi Ijumaa kwa saa za England.