Ni Machi 18, 2024 ambapo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Mohammed Ali Kawaida(MCC) akizungumza na maafisa usafirishaji maarufa kama Bodaboda akimnadi Mgombea Udiwani anayetokana na Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Udiwani katika kata ya Kabwe Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa.
Mwenyekiti amewasisitiza kuwa wakimpa kura za kishindo mgombea wa CCM Ndg. Sebastian Fedrick Kasagama kero zote zinazowakabili wananchi wa Kabwe zipo ndani ya uwezo na zinatekelezeka ndani ya muda mfupi waiamini Chama Cha Mapinduzi kwa maendeleo ya kweli.