Klabu ya Geita Gold Fc kutokea Geita mapema leo imetembelea uwanja wao unaondelea kujengwa katika kata ya Magogo Eilayani Geita na kujionea hali halisi ya ujenzi huku ujenzi huo ukifikia asilimia 95 ya ujenzi mpaka sasa.
Akizungumza mbele ya klabu hiyo Mhandisi Juma Nyajawa kwa kushirikiana na kampuni ya GGML ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo amesema mpaka sasa wangekuwa wamekwisha kukamilisha uwanja huo huku akitaja sababu ya kukosekana kwa udongo ndani ya uwanja huo.
Aidha Mhandisi Nyajawa amesema hadi kukamilika kwa uwanja huo kutachukua kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa kwani changamoto waliyokuwa nayo tayari imekwisha kutatulika.
ULINZI MKALI KWENYE MSAFARA WA RAIS SAMIA NCHINI OMAN