Ni April 7, 2023 ambapo Uongozi wa CRDB Bank Foundation ukiongozwa Mkurugenzi Mtendaji wake, TullyEsther Mwambapa umemtembelea na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT, Brenda Msangi. Mazungumzo hayo yamejikita katika kutazama maeneo ya ushirikiano baina ya taasisi hizo ambazo zote zinalenga kukuza ustawi wa jamii.
Katika kipindi cha mwaka 2022, Hospitali ya CCBRT ilikua ni moja kati ya wanufaika wa CRDB Bank Marathon ambapo zaidi ya Milioni 200 zilikabidhiwa kwa hospitali hiyo ili kusaidia matibabu ya akina mama wenye ujauzito hatarishi.