Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka watu mbalimbali duniani wakiwa wanaelekea kusherehekea sikukuu za Christmas kwa waumini wa dini wa kikristo na sikuku ya mwaka mpya, wameendelea kutoa misaada ikiwa ni lengo la kufurahi na watu wasiojiweza wanaolelewa katika vituo maalum.
Kituo cha Kulelea Wazee na Walemavu sambamba na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na wanaoishi mazingira magumu cha Umra wamepokea msaada wa mifuko ya unga wa ngano kutoka kwa Kampuni ya Camel Flour ikiwa kama sehemu ya kujumuika nao wakati huu wa kusherehekea sikuku za mwisho wa mwaka.
Kampuni hiyo, imekabidhi mifuko 20 kwa Kituo cha kulelea wazee na walemavu Kigamboni na Mifuko 20 kwa Kituo cha watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Umra, akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Biashara na Maendeleo kutoka Camel Flour Tawaqal Sumba amesema wanashukuru kwa mapokezi mazuri waliyoyapata kutoka katika Kituo cha Wazee na Umra na wamefurahi kwa hilo.
Tawaqal amesema, huu ni mwanzo katika kurudisha walichonacho kwa jamii na wataendelea zaidi, kwa upande wa Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kulea Wazee, Frank Munuo amesema wameshukuru sana kwa msaada huo kutoka Kampuni ya Camel Flour ambapo mifuko hiyo itawasaidia katika kuendelea kuwalea wazee hao sambamba na Walemavu.
Kituo cha Umra kina jumla ya wazee 27 wanawalea katika nyumba hizo ambazo zilijengwa mwaka 1973-75 na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo kwa sasa wanalea wazee na walemavu
Wa Ukoma, wasiosikia, wajane, wasioona na afya ya akili, msimamizi wa Kituo cha Umra, Rahma Kishimba amesema wana jumla ya watoto 117 wanaotoka kuishi kwenye mazingira magumu wengine wakiwa ni yatima wanaozanzia umri wa miaka 2 hadi 15.