Wananchi wa Kibondo mjini Mkoani Kigoma wameanza kupata huduma ya maji safi baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa chujio kwa gharama ya shilingi milioni 560 na kuwaondoa katika adha ya kutumia maji yaliyokuwa na matope.
Chujio hilo limejengwa katika mradi wa maji wa Mgoboka ambao Waziri maji, Jumaa Aweso ametembelea kukagua na kupongeza jitihada hizo ambazo zimewaondolea adha ya kutumiamaji yasiyo safi wakazi takribani elfu arobaini wa Kibondo Mjini.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na @ayotv_ wameeleza suala hilo limekuwa ni suala la kihistoria kutokana na changamoto waliyokuwa wakikabili hasa kipindi cha masika ambapo uchafu wa maji ya bombani uliongezeka na kusababisha hata magongwa ya tumbo na kuharisha.
Kwa upande wake Waziri wa Maji @jumaa_aweso ambae ampongeza mradi huo ameahidi kutoa fedha shilingi milioni 200 kwaajili ya umalizaji wa tenk la majia ambalo sasa litawezesha kuondo changamoto ya upungufu wa uhifadhi wa maji.
Katika hatua nyingine Waziri wa maji Jumaa Aweso ameendelea kutua ndoo kichwani kwakuzindua miradi miwili ya maji kwanza katika Kijiji cha chilambo wilayani Kakonko na kisha Kijiji cha Kitahana wilaya Kibondo miradi yote ikiwa na thamani ya zaidi ya bilioni moja.