Ni June 4, 2022 ambapo Taasisi ya Mama ongea na Mwanao inayoongozwa na Mugizaji Steve Nyerere walipata mwaliko katika ofisi za Balozi wa Italia nchini.
Akizungmza na Millardayo.com & Ayo TV Steve Nyerere alisema..‘Hii Fursa kubwa kwetu kwani kwani msanii lazima ajiweke karibu na balozi mbalimbali na tumeanza na Italia na mengineyo yanakuja, lengo ni kuhakikisha wasanii wa ndani wanaitangaza vyema nchi yetu’- Steve Nyerere
‘Leo tumekutana na Viongozi hapa kama mlivyoona wasanii mbalimbali walivyotumia hii nafasi ya kujifunza na kubadilishana mawazo na watu wa Ubalozi huu kwahiyo Mama Ongea na Mwanao inamfungulia Dunia’- Steve Nyerere
Tazama hapa picha mbalimbali kutokea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Balozi za Italia nchini Tanzania