Leo tarehe 25 Juni, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. @napennauye (Mb), amekuwa Mgeni Rasmi katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumpokea Mhashamu Askofu Mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu, Papa Francis kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.
Misa Takatifu imefanyika kwenye Kituo cha Hija cha Ifucha na kuhudhuriwa na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa Dini.