Katika Picha ni Ziara ya mafunzo ya wajumbe wa bodi ya Usalama wa Raia Saccos katika kiwanda cha Uzalishaji nguo na vifungashio cha A to Z kilichopo Jijini Arusha leo Agosti 15,2024.
Ambapo mbali na ziara hiyo Mwenyekiti wa bodi hiyo Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda amekipongeza kiwanda hicho na amewaomba kushirikiana na usalama wa Raia Saccos ambapo kupitia Mtandao wa Polisi wanawake watazalisha taulo za kike na kuzisambaza mashuleni ili kuwasaidia watoto wa kike wanapata changamoto katika siku zao za hedhi.