Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho katika majukumu yao ya timu ya taifa. Neymar na Coutinho wote walianza kuitwa katika timu ya taifa ya wakubwa ya Brazil mwaka 2010, ila Neymar ameshacheza mechi 66 na kufunga magoli 44.
Wakati Philippe Coutinho amecheza mechi 12 akiwa timu ya taifa ya Brazil na kufunga goli moja pekee, Coutinho aliachwa kuitwa katika timu ya taifa ya Brazil kwa muda kidogo kabla ya miezi 12 iliyopita kuanza kuitwa tena.
Neymar na Coutinho walipiga picha yenye pozi kama picha yao ya zamani wakati wanacheza timu ya vijana ya Brazil, Neymar aliiweka picha hiyo katika account yake ya Instagram na kupata likes milioni moja.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos