Silaha zaidi ya 5000 zilizokua zinamilikiwa kiholela zinatarajiwa kuteketezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene leo katika viwanja vya kulenga shabaha vya JWTZ Kunduchi.
Uteketezaji wa silaha hizo unafanyika baada ya kufanyika msako wa kuzikamata kutoka kwa Majangili na Wananchi wa Mikoa mbalimbali kutokana na kutengenezwa kiholela na kutokuwa na vibali.