Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi million 5 kwa familia ya kijana Brayan Nguyaine aliyefariki dunia April 11 2024 wakati akiwaokoa wanafunzi kwenye ajali ya gari ya wanafunzi ya shule ya ghat Memorial iliyotokea katika kata ya Sinoni Mkoani Arusha nakusababisha vifo vya wanafunzi nane
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtehengerwa ametoa kauli hiyo wakati wakuaga miili ya watu hao katika uwanja wa sinoni uliopo Mkoani Arusha nakusema kuwa Rais amefurahishwa na kitendo kilichofanywa na shujaa huyo
Pamoja na hayo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Juma Hamsini amesema kuwa serikali imegharamia mazishi ya watu wote 9 ikiwa ni pamoja na kutoa rambirambi ya shilingi Million moja kwa kila familia