Katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimezitaka Taasisi za Kiserikali na Binafsi kuvisaidia Vituo vya Kulelea Watoto Yatima ili kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.
Akizungumzia hatua hiyo jijini Dar es Salaam kupitia Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Baraka, Mwenyekiti wa TUGHE Taifa, Jane Madette ambaye ni Makamu Mwenyekiti amesema;
“Sisi kama TUGHE huwa tuna utaratibu wa kuelekea siku ya Wanawake Duniani kwenda kwenye vituo na watu wenye mahitaji maalum kutoa sadaka zetu na leo tumetoa vitu mbalimbali ikiwemo,
“Mchele Kilo 100, Sukari, Unga Kilo 150, Sabuni, Maji na Juice lengo kuonyesha hawa watoto tunawajali, hivyo tunatoa wito kwa taasisi na watu wengine kujitolea,”.
Naye Georgina Chirwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati za Wanawake Dar es Salaam TUGHE amesema… “Tumekuwa tukisaidia jamii na kutoa misaada katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambapo leo tumetembelea kituo cha Busara hapa Kitunda,”.
Kwa upande wake Mlezi wa Kituo hicho, Mohammed Sharia Hassan Mlezi Msaidizi amesema… “Tumegawanyika makundi mawili, hawa waliokaa ni watoto wadogo ambapo kuna wavulana na wasichana ambao hawawezi kuathiriana, wale wakubwa tumewapeleka Kigamboni ila hawa wadogo wapo hapa, TUGHE hongereni sana kwa kutupatia msaada huu, hapa tuna watoto 24, wakike 12 na wakiume 12. Tunaziomba taasis zisisite kutusaidi,”.