Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Kagera Cde. *Faris Buruhani,* tarehe 16/01/2024 ameongoza Kikao cha Kawaida cha Baraza la UVCCM UVCCM Mkoa wa Kagera. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa ROYAL HOTEL Wilayani Missenyi.
Pamoja na mambo mengine, Baraza la UVCCM Mkoa wa Kagera limetoa Tamko lenye maazimio makubwa manne ikiwa ni pamoja na kumpongeza sana *Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* Kwa Kazi kubwa anazozifanya za Kuimarisha Demokrasia nchini, Kuinua Uchumi wa Taifa letu kupitia miradi mikubwa na ya kimkakati.
Vile vile, Baraza la UVCCM Mkoa limewapokea Wanachama wapya *193* kutoka kata ya Mabale ambao hapo awali walikuwa wanachama na viongozi
wa CHADEMA kutoka katika kata hiyo ya Mabale. Wanachama hao wamepokelewa na kukabidhiwa Kadi za CCM na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera *Cde. Faris Athuman Buruhani.
Aidha kupitia Mikakati mikubwa iliyowekwa na Baraza la UVCCM Mkoa, Mbaraza wa Mkoa Cde. Leodiger Kachebonaho amekabidhi *Simu 10 aina ya SAMSUNG GALAXY A14.* Zenye thamani ya *Tsh. 4,500,000/= na kuzigawa kwa Wilaya zote 8 za Mkoa wa KAGERA. Kwaajili ya Kuongeza Kasi ya Kusajili Wanachama katika mfumo wa Kieleteoniki.
Mwisho, Baraza la UVCCM Mkoa limeazimia ndani ya mwaka huu wa Uchaguzi wa *2024* kuhakikisha Vitongoji, Vijiji na Mitaa yote, ndani ya mkoa wa Kagera inaendelea kuwa ndani ya himaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Wakubwa na wananchi haswa vijana walitutuma kazi na kazi inafanyika Mkoa wa Kagera. 💪🏾🙏🏾. Jana niliweza kukabidhi simu 10 katika Baraza la UVCCM Mkoa wa Kagera zenye thamani ya 4,500,000. Na Mwenyekiti wetu wa UVCCM @farisburuhan , Aliweza kuzikabidhi kwa makatibu katika kila Wilaya ya Mkoa wa Kagera”- Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM, Leodger Leonard Kachebonaho
“Lengo kubwa la hizi SIMU MPYA 10 ni za Usajili na Kujipanga kimkakati kuongeza wanachama Wapya kupitia usajili wa Wanachama wapya kwa njia ya Elektroniki”- Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM, Leodger Leonard Kachebonaho