Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo July 30, 2021 amechanjwa chanjo ya Uviko 19 katikà viwanja vya kituo cha Afya Mkoani Kibaha
Kunenge amewaasa Wanachi wa Mkoa huo kuwa ugonjwa upo na kuwataka kuchukua tahadhari wakati wote, amewataka Kuvaa barakoa, kunawa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo lazima.
Amemshukuru Mhe Rais kwa kupata chanjo, “nimechanja kwa hiari yangu mwenyewe mpaka sasa najisikia vizuri sijaona shida yeyote”
“Wananchi waje wachanje kwa hiari yao tunachotafuta ni salama” tumepata chanjo kidogo tunaendelea kuratibu upatikanaji wa nyingi zaidi na tutaitoa bila usumbufu. Chanjo hii kwa sasa itatolewa kwa makundi ya Kipaumbele” alisema Kunenge.
WAZIRI AMPINGA GWAJIMA KUHUSU CHANJO “GWAJIMA NI KUMUELIMISHA TU”