Mchekeshaji Peter Mollel (Pierre Liquid) ambaye alipata maambukizi ya corona amethibitisha kuwa tayari amepona na kuruhusiwa huku akiwataka Watanzania kutoogopa na waende Hospitali pale wanapoona dalili.
“Niliwekwa karantini Amana nikawa nameza dawa, pia mazoezi yamenisaidia sana nilikuwa siwezi kuhema ila baada ya mazoezi nikaanza kuhema, mbavu zilikuwa zinanibana zimeacha, sijajifukiza kwasababu mimi namuamini Mungu”- Pierre