Leo January 15, 2018 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Temeke ili kuona jinsi wananchi wanavyopokea huduma za afya.
Kati ya mambo aliyozungumza ni pamoja na suala la msongamano wa wanawake wajawazito kulala chini pamoja na kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda kimoja na kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salamaa amekwishafanya mazungumzo na mfadhili hivyo watawasiliana ili lijengwe jengo moja la ghorofa nne la wakinamama wajawazito ili kupunguza msongamano.
Ameeleza pia kuwa ndani ya mwezi huu serikali itapeleka fedha katika hospitali hiyo ya Temeke ili kununua vifaa kwaajili ya chumba cha upasuaji ambacho ni kimoja tu hospitalini hapo.
Ajali ya HIACE iliyoua 11 Kagera, aligonga Malori mawili.
Cyprian Musiba atangaza kumshitaki Tundu Lissu