Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amewaasa Wakurugenzi Watendaji na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali nchini kuitumia Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Kwamfipa Mkoa wa Pwani, kuendelea kujielimisha ili kumpunguzia kazi Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali (CAG).
Pinda amesema hayo kwenye ufunguzi mafunzo ya 19 ya siku sita kwa Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini, katika Shule ya Uongozi wa Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha ambapo amesema Shule hiyo itumike vizuri kuwajengea uwezo Viongozi mbalimbali..
Amesema Viongozi hao waende kusoma katika Shule hiyo wapigwe msasa wa mara kwa mara ili kumpunguzia CAG kazi kwa Viongozi wote kufanya kazi katika malengo ya aina moja.
“Kunatakiwa kuwe na kozi fupifupi kwa sisi tulio huku Serikali kwani Kuna ubaya gani Ma-DC wote tukutane hapa na Viongozi wote wa Taasisi zinazohusu uendeshaji wa nchini kwa ujumla na mambo yote yanayohusu makatazo kwa Kiongozi”
“Wakurugenzi njooni hapa tena wote mmetokana na Chama kinachoongoza piga msasa hawa watu ndipo hautasikia CAG akipiga kelele tena”
“Nasisitiza uadilifu na kuacha maovu ambayo yanaathiri jamii kwa ujumla ndiyo maana CAG akitoa ripoti yake inakua imejaa madudu mengi yote haya ni upungufu wa maadili kwa baadhi ya Viongozi ” amesema Pinda.
https://www.youtube.com/watch?v=udP-PgkbNHg