Mwanariadha Oscar Pistorius ameendelea kukaa kwenye headlines!! ikiwa ni siku chache tangu hukumu yake itoke, na kushtakiwa kwa mauaji ya kukusudia, kuna hiki kingine kimenifikia kuhusu kesi yake.
Jaji anayesimamia kesi yake Aubey Ludwaba ametoa dhamana kwa mwanariadha huyo hadi April 18, 2016 huku akisubiri kuhukumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp, ambapo kifungo kinaweza kufikia miaka 15.
Pia Pistorius ametakiwa kulipa kiasi cha dola 700 kama dhamana na ataendelea kutumikia kifungo cha nje ambacho masharti yake anaruhusiwa kuondoka eneo analoishi kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 6 mchana na kwa umbali usiozidi km.20.
Kwa mashtaka mapya yanayomkabili huenda kifungo chake kikafikia mpaka miaka 15 jela badala ya ile mitano aliyohukumiwa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.