Baada ya kuahirisha kesi kwa muda Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite amegoma kujitoa kusikiliza kesi inayomkabili Joseph Mbilinyi ‘SUGU’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga.
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli katika mkutano uliofanyika December 30, 2018.
Leo January 25, 2018 Sugu na Masonga waliwasilisha ombi Mahakamani wakimtaka Hakimu Mteite ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye.
Akijibu hoja hizo Hakimu Mteite amesema hoja zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria hivyo hawezi kujiondoa katika kesi hiyo.
Baada ya Hakimu kukataa kujitoa, Mawakili Boniphace Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo.
Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta Mawakili wengine.
Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi February 2, 2018 na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.
BREAKING: SAID AMWAGA MACHOZI BAADA YA SCORPION KUHUKUMIWA MIAKA 7