Mtoto wa miaka 13 huko Los Angeles Marekani, ‘ameponea chupu chupu’ kupoteza maisha baada ya kudumbukia kwenye shimo kubwa la maji taka yenye sumu.
Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Jesse Hernandez anadaiwa kukaa kwenye shimo hilo kwa takriban saa 12 jambo ambalo timu ya waokoaji imesema haikuwa rahisi mtoto huyo kutopoteza maisha.
Zoezi la kumuokoa mtoto huyo limefanywa na timu ya takriban watu 100 ambao walilifanyia ukaguzi mkubwa shimo hilo la mita 730.
Inaelezwa kuwa mtoto huyo alikuwa akicheza juu ya mbao ambazo ndizo zilikuwa zimefunika shimo hilo na ghafla mbao moja ilivunjika na kusababisha mtoto huyo kudumbukia mita 8 kwenye shimo hilo.
Mbowe na Viongozi CHADEMA walivyofikishwa Mahakamani
https://youtu.be/udqezlAsIyQ