Najua kama ni mtumiaji wa usafiri wa ndege utakuwa umekutana na taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege inataka kupaa na kutua ila huenda ikawa hufahamu ni kwanini haswa unatakiwa kufanya hivyo, na inawezekana ulishajiuliza pia ina maana usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.
Vibrations au miungurumo ya simu na vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa kuhusiana na swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?.