Hali ya taharuki imetokea katika wa Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya Desember 29, 2018 wakati polisi walipokamata chupa ya pombe kali aina ya Vodka kutoka Urusi, chupa yenye umbo la bunduki aina ya AK-47.
Polisi katika uwanja huo walikamata chupa hiyo ya pombe kali kwa jina ‘Kalashnikov vodka’ katika eneo la kuwasili wageni.
Tukio hilo lilianzia kwenye mashine ya ukaguzi katika uwanja huo wa ndege ambapo polisi walinasa kifaa kilichokuwa na muundo na umbo la bunduki.
Kulingana na Neel Akber aliyefichua uwepo wa tukio hilo amesema iliwachukua muda mrefu maafisa wa polisi kugundua haikuwa bunduki ya ‘AK-47’ bali ni chupa ya pombe kali.
Uchunguzi wa polisi hatimaye ulibainisha kuwa, pombe hiyo ilikuwa safarini kuelekea Bangui kutoka Russia na ilikuwa kwenye ndege ya shirika la Qatar Airways wakati wakiikamata.
Polisi hatimaye waliipeleka chupa hiyo kwenye maabara ya serikali kuchunguza zaidi.
Uchunguzi wa millardayo.com umebaini pombe hiyo aina ya ‘Kalashnikov’ ni mojawapo ya pombe inayopendwa Russia na imepewa jina hilo kumkumbuka Mikhail Kalashnikov ambaye alikuwa Jenerali wa jeshi nchini humo aliyefariki December 23, 2013.
VIDEO ILIYOWANASA BABU SEYA NA WANAE WAKIINGIA IKULU LEO
UAMUZI WA TCRA KWA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOKIUKA KANUNI ZA UTANGAZAJI