Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Paul Kisabo amezungumza na AyoTV na millardayo.com kuhusu kufungua maombi katika Mahakama Kuu ya kutaka jeshi la Polisi limpeleke Abdul Nondo Mahakamani ambapo amegusia wao kwenda Polisi na kuambiwa Nondo hayupo.
“Tulienda Polisi Makao makuu kuuliza kama Nondo yupo pale kama yupo tumuombee dhamana au wamlete Mahakamani, tumeuliza mapokezi Polisi wametuambia Nondo hayupo, sisi hatujaonana nae” -Paul Kisabo