Wakati Tanzania headlines mbalimbali za Viongozi wa dini kuzungumza siasa Makanisani zikiendelea, leo Katibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Humphrey Polepole na amekubali kuzungumzia hiki kinachoongelewa na baadhi ya viongozi wa dini kupitia Azam TV.
Kwenye sentensi zake za mwanzo Humphrey Polepole amesema>> ‘Hakuna mtu amezuiliwa kuongea kwenye nchi ya Tanzania, hakuna mtu ametishwa kwa kusema ukweli katika nchi ya Tanzania na hasa katika uongozi wa awamu ya tano wa Ndugu John Pombe Magufuli’
Sehemu nyingine ya mahojiano yake amesema>> ‘Usihukumu hujafanya uchunguzi, huna haki ya kuongea hujafanya utafiti na mwisho huna takwmu huwezi kujenga hoja, anayesema mtu kazuiliwa kuzungumza uhuru wake wa maoni nadhani atakua na tatizo jingine,ambacho nakifahamu kuzungumza lugha ya matusi kwa mujibu wa jkatiba yetu na sheria zetu ni makosa’.
1/2 … #AzamNews Hii ndiyo kauli ya msemaji wa @ccm_tanzania @hpolepole kuhusu katazo la serikali kwa viongozi wa dini kuzungumzia siasa. Asema hakuna anayezuiwa kutoa maoni yake. pic.twitter.com/7PVJ5E3qkJ
— AzamTV (@azamtvtz) December 28, 2017
2/2 … #AzamNews Hii ndiyo kauli ya msemaji wa @ccm_tanzania @hpolepole kuhusu katazo la serikali kwa viongozi wa dini kuzungumzia siasa. Asema hakuna anayezuiwa kutoa maoni yake. pic.twitter.com/vLJFWNHpUe
— AzamTV (@azamtvtz) December 28, 2017
POLEPOLE: ‘Lengo la Uchaguzi huru ni kukirejesha Chama kwa Wanachama’.