Power Breakfast ilikuwa hewani asubuhi ya leo February 26, mgeni rasmi ambaye alipata nafasi ya kufanya mahojiano ni Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paul Makonda ambaye vyombo vya habari vilikuwa na headlines nyingi kuhusu yeye tangu siku ambayo alitangazwa kuwa DC mpya wa Wilaya hiyo.
Cha kwanza kukizungumzia ni historia ya maisha yake; “Nina miaka miwili nimekaa Sinza lakini nimekaa Survey miaka miwili.. kwa hiyo nina miaka minne.. Nilikuwa natoka naenda Chuo na kurudi Dar..”
“Mama yangu ndio msomi kuliko wote nyumbani kwetu, darasa la saba halafu mzee hakufanikiwa kuanza hata darasa la kwanza.. Nimepita kwenye mfumo ambao ulinilazimisha kuwa kiongozi wa maisha ya kwangu mwenyewe, sikuwahi kufikiri kumfikiria mtu kuamua kwa niaba yangu..”
Safari yake kuwa kiongozi ilianzia huku; “Ndiye niliyefanikiwa kuwa Rais wa Serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vyote Tanzania mwaka 2011-12.. Moja nilisaidia kutokomeza mgogoro wa mgomo uliokuwa unasababishwa na Bodi ya Mikopo.. Nilifanya kazi ya kushirikisha Bodi ya Mikopo ikubali kuajiri Watumishi wa Bodi ya Mikopo kwa kila Chuo. Pili kulikuwa na shida ya kuhama, tukafanikiwa kutengeneza mfumo ukiwa unasoma accounts Arusha ukahama na accounts yako mwaka wako ukaja ukaendelea na IFM darasa lilelile na mwisho ukamaliza..”
Hapa anazungumzia ishu ya kupingwa na watu wengi baada ya kuteuliwa; “Huo ndio uhai wa fikra, haiwezekani watu wote waunge mkono mambo yote.. Kupingwa kunakufanya wewe uwe kiongozi imara.. ni utamaduni wa kawaida watu kukataa mambo wasiyoweza kuyaona, tuna tabia ya kukubali kitu baada ya kitu hicho kuwa kimeondoka. Haiwezekani wananchi hawakusemi halafu unataka kuwaongoza”
Kuhusu tukio lililoandikwa na Magazeti kwamba alimfanyia vurugu Mzee Warioba; “Tukio lile halijaathiri chochote, limeongeza thamani yangu katika jamii.. Mtu mwingine anaweza akasema hii mbona inaenda kumzamisha kwangu mimi najua ni sehemu mojawapo ya kunisaidia mimi kwenda hatua moja kubwa..”
“Kilichosemwa sicho chenyewe matokeo yake kimenisaidia kunizalishia marafiki kunikaribishia marafiki wengi kuliko maadui.. kila akisema Mzee Warioba hakuna anayeandika mwisho wa siku huwa namwambia mzee wewe kaa kimya.. Inafika kipindi nasema labda kuna Mzee Warioba mwingine, kama Mzee Warioba anasema sivyo lakini kuna watu bado wanaandika maana yake kuna Warioba mwingine ambaye Makonda hamfahamu na Mzee Warioba naye hamfahamu”
Mipango ya Makonda kwenye Wilaya ya Kinondoni; “Leo ni siku yangu ya tatu.. nimejipa muda ndani ya siku 90 naamini Kinondoni itakuwa tofauti na jinsi ambavyo watu wanavyoitazama“
Nimeirekodi yote kwa ajili yako mtu wangu, bonyeza play hapa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook