Kuna mtu unaweza kumzungumzia mambo yake binafsi akakaa kimya tu asiongee lolote lakini wengine huwa hawapendi kabisa.. ishu ya kuongelewa madeni yake kwenye Kikao cha Bunge, Mchungaji Peter Msigwa hakuipenda.
“Nampongeza Waziri wa Fedha, kwa kweli anafanya kazi yake vizuri.. Nchi hii iko taabani fedha hakuna lakini Waziri bado yumo tu.
Na hata Msigwa angepewa Wizara hii kama fedha isingekuwepo nae angekuwa hoi vilevile… Sasa Msigwa anashangaa Serikali inadaiwa yeye mwenyewe juzi kaletewa makaratasi anadaiwa… Kudaiana ni jambo la kawaida“>>>– Mbunge Said Mtanda.
Mbunge Peter Msigwa akawasha kipaza sauti; “Mbunge anaezungumza anaingilia mambo binafsi, masuala ya madeni yangu asiyajadili hapa. Hili ni Bunge tunajadili mambo ya Nchi, anajuaje madeni yangu? Huku ni kuniingilia, aache kabisa kuingilia mambo yangu”>>>– Mbunge Peter Msigwa.
Sauti ya Majibizano hayo iko hapa mtu wangu, nimeitoa kwenye Kikao cha Bunge kinachoendelea June 15 2015 Dodoma
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.