Kwa muda mrefu zimekuwepo taarifa kuwa mwenyekiti wa club ya Yanga SC Yussuf Manji na mzee Akilimali hawaelewani, wengine wakisema kuwa ni kwa sababu mzee Akilimali anapinga wazo la Yussuf Manji kuikodisha Yanga kwa miaka 10.
Leo Mzee Akilimali amezungumzana AyoTV kuhusiana mahusiano yake na Manji, vipi wameongea lini kwa mara ya mwisho, ana mpinga Manji kweli? akikutana na Manji atamwambia nini?
“Kwa mara ya mwisho kabisa mimi kuongea na Manji ilikuwa majira ya saa sita mwaka jana, kabla hajaandika hiyo barua ndio alinipigia na kueleza mawazo yake ya kutaka kujiuzulu, nikamuomba sana tafadhali mwanangu usijiulu kwa haya”
Kocha amewaondoa wachezaji wa Simba, katika kikosi cha Taifa Stars