Katika matukio ya mauaji yaliyotikisa Tanzania hivi karibuni ni pamoja na tukio la mauaji ya watu wanane Tanga na mengine yaliyofanyika msikitini mkoani Mwanza.
Leo June 2016 Jeshi la polisi Dar es salaam kupitia kwa Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro ametoa taarifa ya kuuwawa kwa majambazi wawili wanaodaiwa kuhusika na matukioa hayo.
Sirro amesema jeshi hilo limemuua jambazi sugu aliyejulikana kwa jina la Salum Mhangwa aliyedaiwa kuhusika na mauaji msikitini mkoani Mwanza na kufanya matukio ya kiuhalifu, jambazi huyo alikutwa na bomu la kurusha kwa mkono.
Jeshi hilo pia limemuua jambazi sugu aliyedaiwa kuhusika na mauaji ya watu nane mkoani Tanga ambaye alikuwa anatumia silaha kali kama bomu la kurusha kwa mkono na bastola ambavyo alikutwa navyo.
ULIKOSA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KWENYE UZINDUZI WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA POLISI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB INSTAGRAM YOUTUBE