Polisi waliendesha msako kwenye Hoteli mbalimbali India kama wiki moja hivi iliyopita, kisa cha kuendesha msako huo walidai kwamba wenyeji wa eneo la Mumbai walilalamika kwamba kuna mambo maovu yanafanyika kwenye maeneo yao, Polisi wakaona waingie mtaa kwa mtaa kumalizana na wanaofanya hayo mambo !!
Wapendanao zaidi ya 20 walikamatwa katika msako huo, lakini kibao kikageuka baada ya Polisi kufanya msako na kuwakamata wapendanao hao katika Mahoteli mbalimbali badala ya mtaani !
“Nimeshindwa hata kutoka nje ya nyumba yetu, wazazi wangu hawajaongea neno hata moja na mimi toka kumekucha… Mimi sijiuzi, ni mtu mzima na nilitoka na mpenzi wangu ambae natakiwa kufunga nae ndoa mwezi ujao”—mmoja wa wasichana walionaswa kwenye msako huo alilalamika.
Malalamiko yamekuwa mengi sana kwenye Mitandao ya Kijamii India baada ya hii ishu japo Kamanda wa Polisi Mumbai, Rakesh Maria amepinga msako huo kufanyika kwenye Mahoteli >>> “Kama watu wazima wawili wakiwa ndani ya chumba cha Hoteli kwa mambo yao sisi haituhusu”
Moja ya website kubwa India imelaani pia hiyo ishu na hii ni moja ya sentensi zilizokosoa kitendo hicho >>> “Hakuna Sheria inayokataza watu ambao hawajaoana kuwa kwenye chumba cha Hoteli pamoja”
Hizi ni baadhi ya Tweets kwenye zilizoweka Trend kulaani Polisi.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos