June 2 2016 Jeshi la polisi nchini lilitoa tamko lililolenga kuzuia mikutano, maandamano ya kisiasa nchini kutokana hali za kiusalama kutokuwa sawa.
Leo July 09 2019 Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu tamko la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kuwa tamko hilo lililenga kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na tamko hilo halikupiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.
Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika.
ULIKOSA HAYA MAMBO MUHIMU YA KUYAJUA ILI USIPATIKANE KWENYE MIKONO YA POLISI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI