Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema linafuatilia Watu wanaoweka miungurumo ya milipuko katika magari na pikipiki zao na kupelekea kuleta mshtuko kwa Jamii.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, SACP. Wilbroad Mutafungwa amesema wamepokea malalamiko kutoka kwa Raia wakieleza kukerwa na milipuko hiyo na kwamba tayari wamefanikiwa kuwakamata Vijana wawili waliobadili mifumo ya magari yao na kupelekea kero pindi wanapotumia barabara.
Mutafungwa pia ametoa onyo kali kwa Vijana wanaofanya hivyo kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria ya usalama barabarani kifungu namba 39 (1), na zoezi la kuwasaka wanaofanya hivyo bado linaendelea.