Jeshi la polisi Zanzibar limekanusha juu ya madai yanayosamba mitandaoni kua limefanya utekaji katika kwenye duka la vileo ZMMI (Migoz) Migombani Mjini Unguja na kufafanua kua mafisa wa bodi ya vileo zanzibar walikua katika operesheni yao ya kawaida na kugundua kua kuna taratibu ambazo hazikua sahihi ndipo walipoondoka na watu hao kwa mahojiano
DCP. Zuberi Chembera Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar amesema Jeshi la polisi halihusiki na shtuma hizo na limekanusha vikali na kwamba pale hapakua na utekaji nyara na hali iliojitokeza ilikua ni hali ya utendaji wa kisheria na kihalali wa mamlaka hiyo juu za usimamizi wa uzwaji wa vileo Zanzibar
” Maafisa wa Bodi ya vileo Zanzibar wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida za kazi walifika dukani hapo kutokana na kupata taarifa za shtuma kwamba kwenye duka hilo wanakiuka sheria za uthibiti wa vileo hapa Zanzibar ,walipofika pale wakati wa mahojiano kati ya maafisa hao na uwongozi kukatokea kutoelewana na kurushiana maneno hivyo waliondoka na viongozi hao—DCP. Zuberi Chembera “